MALEZI HAYA NDIO YAMETENGENEZA VIONGOZI TULIONAO SASA! (UTAWALAUMU?)

MALEZI HAYA NDIO YAMETENGENEZA VIONGOZI TULIONAO SASA! (UTAWALAUMU?)

Kama umezaliwa kabla ya mwaka 1990 utakubaliana na mimi kwa aina hii ya malezi uliyolelewa nayo!

1.Mzazi ndiye Mungu, yaani hata kama umefundishwa kwamba anga ni la bluu, mzazi akikuambia anga lina rangi ya njano inabidi ukubali!
(matokeo yake viongozi hawakotayari kukosolewa)

2. Nyumbani ni kwa ajili ya yeyote ilimradi tu awe ni ndugu, ndugu yeyote  anaweza  kuja kukaa kwa muda wowote hata kama alifukuzwa kwao hukuna haja ya kuwa na wasiwasi nae maadam ni ndugu yetu!
 (matokeo yake, mgeni toka nje akija, No problem! Ni rafiki zetu sana hawa, mpe ardhi)

3.Mdogo kwenye familia ndiye atakaesingiziwa kafanya uharibifu wowote nyumbani,  mpaka atakapokuwa na uwezo wa kujitetea!
(Matokeo yake wenye vyeo wakitaka “kula” wanatumia mgongo wa watu Fulani wa chini ambao hawana sauti)


Sababu Zingine

4. Mkubwa kwenye familia ndiye atakaeadhibiwa na kupewa lawama kwa kile mdogo alichofanya mdogo anaachwa.

5. Wazazi watakuita ukiwa nje unacheza, au unasoma ili wakutume uwachukulie kitu kilichopo mita chache kutoka walipokaa.

6. Sahau Suala la kusifiwa, Ukipata B darasani utaambiwa kwani aliyepata A ana vichwa vingapi?

7. Mtoto hafundishwi elimu ya  uhusiano anapobalehe. Yeyote anayeonekana nae huitwa rafiki na mzazi hana muda wa kufuatilia. Unachoambiwa ni “Usituletee aibu nyumbani”

8. Mtoto wa kike hafundishwi chochote kuhusu maisha na baba! Mpaka awepo mama au shangazi

9. Kuna Kinywaji Kabatini? Au Kuna kuku anachinjwa? Oooh basi ujue leo kuna mgeni anakuja!


10. Lazima usomee kozi aliyosomea Yule msomi wa kijijini kwenu. Hii ni amri imetoka kwa baba.

3 comments:

  1. Kweli aisee nimeipenda hii!

    ReplyDelete
  2. Asante, upo sahihi ha ha ha , Hiyo ya 6 nilikuwa nayo miaka miwili nyuma kwa watoto wangu. Nimebadilika naona matunda mazuri.

    ReplyDelete
  3. Da! nmeinjoy sana big up kwako💪

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu